Glorypascal pfp
Glorypascal

@glorypascal

⚠️Kwanini unapaswa Kuwekeza Badala Ya Kuweka Akiba Tu ??? sababu ni hii.... Kuweka AKIBA tu maana yake ni kuiacha pesa yako ilale. Inakaa tu. Haisaidii. Haifanyi kazi yoyote Na cha kusikitisha zaidi, mfumuko wa bei unaila taratibu. Lakini... KUWEKEZA maana yake ni kuipeleka pesa yako kazini. Inaamka. Inazalisha. Inafanya kazi usiku na mchana — na inaanza kukuandalia maisha ya ndoto zako. Sasa jiulize: Unataka pesa yako ilale kwenye akaunti isiyo na faida? Au unataka iende ikapambane sokoni, ikuzalie faida kila siku? Kwa sababu ukweli ni huu: Ukiishia kuweka akiba Tu Pesa hubaki pale pale. Lakini.. Ukiwekeza Pesa Zako Zinaanza kuzaliana Kwahiyo Chaguo ni lako. Uendele kuweka Akiba au uanze Kuwekeza
0 reply
0 recast
0 reaction