@glorypascal
_Tofauti ya 'Being Rich' na 'Being Wealthy' — Na Unapaswa Kutafuta Kipi?_
Watu wengi huchanganya maana ya kuwa rich na wealthy, lakini hizi ni vitu tofauti kabisa.
Rich ni mtu anayekuwa na pesa nyingi kwa sasa, lakini anaweza kutumia pesa zote haraka bila akiba au uwekezaji wa kweli. Hali yake inaweza kuwa ya muda mfupi.
Wealthy ni mtu aliyejenga mfumo wa kupata pesa endelevu, anayeweza kupata faida bila kuhitaji kufanya kazi kila wakati. Ana mali, akiba, na uwekezaji unaomlinda hata wakati mgumu.
_Swali lako ni: Unataka kuwa rich au wealthy_ ?
Kuwa rich ni kama kufurahia chakula kizuri mara moja, lakini kuwa wealthy ni kama kuwa na mlo wa kila siku, siku zote.
Katika safari ya fedha, lengo lako liwe kujenga wealth - akiba, mali, na mapato ya passive (kama Gawio kutoka kwenye kampuni).
Hii ndio njia ya kweli ya uhuru wa kifedha. Usikimbilie pesa za haraka, badala yake jifunze jinsi ya kuijenga kwa ustadi!